Mwaka 2017, Rais wa Marekani Donald Trump alitia saini agizo la sera ya anga za juu kuwapatia idhini wataalamu wa anga za mbali wa nchi hiyo kurejea mwezini na mbali zaidi ya hapo.
Shirika la anga la Marekani NASA lilisema litafanya hivyo kufikia mwaka 2028 lakini hivi karibuni utawala wa Trump uliliagiza shirika hilo kurejesha nyuma mpango huo hadi mwaka 2024, kutokana na juhudi zinazofanywa na China kufika mwezini.
Hata hivyo tarehe iliyowekwa inatarajiwa kugongana na muda ambao Trump anakamilisha muhula wake wa pili madarakani ikiwa atachaguliwa tena.
Wakati huu, Nasa inataka kufanya vitu tofauti. Kwenda mwezini ni sehemu ya mpango wake wa kuangazia zaidi sayari nyengine zinazokaribiana na mwezi kama vile Mars.
"Hatuwezi kurudi mwezini na kuacha bendera na nyayo zetu halafu turudi tena huko miaka mingine 50 ijayo ," afisa wa Nasa Jim Bridenstine alisema mapema mwaka huu.
Lakini je Nasa inaweza kufikia muda waliowekewa na Trump kurudi mwezini, ikizingatiwa bado vifaa vingine muhimu havijakuwa kamili na/au vingine vinafanyiwa majaribio?
"Itakuwa vigumu sana kufikia tarehe hiyo," anasema John Logsdon, profesa mstaafu kutioka chuo kikuu cha George Washington DC.
Lakini anaongeza kuwa: " ikiwa hatuko tayari kukubali makosa yoyote basi tusalie ardhini kwa sababu ni vyema tutathmini changamoto itakayotokana na shughuli yenyewe."
Mpango wa mwisho wa safari ya anga za juu ulipewa jina mungu wa kale wa Kigiriki, Apollo.
Itakayofuata itapewa jina la Artemis amabye ni pacha wake, na pia kuna lalama kuhusu hatua ya shirika hilo kuhusisha shughuli hiyo na mwanamke wa kwanza kwenda mwezini.
Nasa ina maafisa 38 ambao ni wataalamu wa anga za juu, 12 kati yao ni wanawake ikiwa ni pamoja na Kate Rubins, ambaye ni mwanabailojia mashuhuri duniani; Jeanette Epps, afisa wa zamani wa kiufundi wa CIA; Serena Aunon-Chancellor, Daktari; na Christina Koch, mhandisi.
Jim Bridenstine hivi karibuni aliiambia CNN: "Ni mtu mwingine tofauti kabisa ambaye ashawahi kufika anga za juu na ameidhinishwa kusafiri kituo cha kimataifa cha anga za mbali".
Stephanie Wilson ana uzoefu zaidi wa kupaisha chombo angani na amewahi kuhusika mara tatu katika safari za majaribio.
Tracy Caldwell Dyson na Sunita Williams, wote wamepaisha ndege mbili katika anga za mbali.
"Hali ilivvyo kwa sasa, tunahitaji uzoefu zaidi unapoangazia utendakazi wa wataalamu hawa zaidi ya wale tunaowafahamu katika historia ," anasema Michael Barratt, mtaalamu wa Nasa ambaye pia ni profesa wa Chuo Kikuu cha matibabu cha Exeter nchini Uingereza.
"Mtaalamu wa leo wa anga za juu anatakiwa kuwa na ujuzi wa kufanya vitu vingi ikwa ni pamoja na kuendesha gari maalum kwa miezi sita, kutembea angani, kutumia roboti na mitambo mingine inayotumia lugha ya Kiingereza na Kirusi na pia awe na uwezo wa kufanya kazi akiwa ametengwa na wezake kwa miezi sita wakati mwingine."
Tayari tuna uelewa mzuri kuhusu mabadiliko yanayokumba mwili wa binadamu wakiwa anga za juu. "Kwa mfano tuseme wanakuwa fofauti kabisa," anasema Barratt, ambaye pia ni Daktari. "Mfumo wa miiili yetu hubadilika, fiziolojia hubadilika, biokemia pia hubadilika.
"Lakini mwili bado huwa na uwezo wa kufanya kazi, hii yo tayari ni hatua kubwa sana."
Wataalamu wa anga za juu watakabiliana na majanga mengi wakifika mwezini. "Japo watachukua miezi sita pekee wanavalia suti nzito, huku wakiwa wamebeba vifaa vizito vya kazi, hali ambayo inachangia changamoto wanazokuabiliana," Barratt anasema.
Wataalamu hao pia huenda wakavunjika viumgo vya mwili wakianguka au kutoka katika vazi lao maalum.
Pia kuna tatizo la vumbi linalopatikana katika mazingira ya mwezini. Wataalamu wa Apollo waliosafiri mwanzo mwezini walikabiliwa na tatizo la kukohoa na wakati mwingine kushindwa kupumua vizuri vumbi lilipoingia kwenye chombo chao cha safari. Kuna haja ya kutafuta suluhisho la kijikinga na vumbi hilo.
Mionzi pia ni moja ya hatari inayowakabili wakiwa mwezini. Mionzi hiyo inawaweka katika hatari ya kupata matatizo ya kiafya kama kupata magonjwa ya moyo na saratani
Mpango wa Wamarekani kurudi tena mwezini ni kutumia mfumo wa chombo kinachofahamika kama Orion.
Utenda kazi wake unasadikiwa kuwa imara zaidi kama vile mfumo wa Apollo ulivyoimarishwa zaidi ya chombo kilichofanyiwa majaribio kwenda anga za mbali.
Watu wengi huhusisha vyombo vingi vya angani na zama za binadamu kutaka kuvumbua wasichokijua katka anga za mbali zinakaa vipi, wakati kulikuwa na hofu uchunguzi huo hautawezekana.
Lakini chombo cha angani kilicho na uzani wa tani 10 kilitumia uwezo wa teknolojia ambayo wengi hawakudhania inawezekana miaka ya 1960, na mpaka sasa teknolojia hiyo inatumika kuvumbua vitu vipya duniani.
"Katika shirika la Lockheed Martin, ambalo linaunda chombo cha Orion Nasa, wahandisi wake wanavaa kifaa maalum masikioni ambacho kinawawezesha kung'amua vitu vingi kupitia mfumo wa kidijitali," anaelezea Shelley Peterson, mkuu wa kitengo cha teknolojia zinazoibuka katika shirika la Lockheed.
Kwa kutumia mwongozo unaotumika katka ulimwengu halisia, mafundi mitambo wanaweza kwa njia rahisi kutoboa shimo au kuweka alama katka sehemu fulani ili kukaza kama au mshipi. Hii ina maanisha hawahitaji kusoma maelfu ya kurusa ya vitabu, hali ambayo inawawezesha kufanya kazi haraka na kwa utaalamu zaidi.
"Tulikua na mtu kwenye chombo cha Orion ambaye anakaribia kustaafu," ansema Peterson. "Ameonesha kuwa huenda akaahirisha mpango huo ili apate fursa ya kukipaisha angani."
Ikilinganishwa na Apollo, "Orion ni pana kutokana na uwezo wake wa kuhimili upepo mkali," anasema Rob Chambers, afisa mkuu anayesimamia mitambo ya kiufundi katika shirika la Lockheed Martin, ambayo inaiundia Nasa chombo cha Orion for Nasa.
Orion ilikuwa sehemu ya mpango wa rais George W Bush wa kurudi tena mwezini uliotangazwa mwaka 2004. Mpango huo ilifutiliwa mbali mwaka 2010 chini ya utawala wa Obama.
No comments:
Post a Comment