Lt Malick Jatta: Mwanajeshi wa zamani Gambia asema Yahya Jammeh alimuamuru kuua
Mwanajeshi mmoja nchini Gambia amekiri kuhusika katika mauaji ya wahamiaji wapatao 50 mnamo 2005 kutokana na agizo la rais Yahya Jammeh, anayearifiwa kuwa alihofia kwamba wanaume hao walikuwa na nia ya kumpindua.
Luteni Malick Jatta alikuwa anatoa ushahidi mbele ya tume ya ukweli na maridhiano TRRC inayochunguza maovu yaliotekelzwa chini ya utawala wa miaka 22 ya Jammeh.
Hapo awali alikiri kuhusika katika mauaji ya mwandishi Deyda Hydara mnamo 2004 kwa agizo la kiongozi huyo wa zamani Gambia.
- Zoezi la kijeshi la Urusi na China lazua tumbo joto
- Jammeh 'aliondoka na $11m' kutoka Gambia
- 'Dawa ya Ukimwi ya Yahya Jammeh karibu iniue'
- Bobi Wine kutangaza azma yake ya kuwania urais Uganda
Jammeh - ambaye sasa anaishi uhamishoni huko Guinea ya Ikweta - amekana kuhusuika katika vifo vya wahamaiji na mwandishi habari huyo.
Deyda Hydara alikuwa muasisi mwenza na mhariri msimamizi wa gazeti la The Point nchini humo.
Jatta alisema alilipwa $1,000 kutekeleza maujai hayo, licha ya kwamba ni mpaka siku ya pili ambapo aligundua kwamba alikuwa amemuua Hydara.
Jammeh alitorokea Guinea ya Ikweta mnamo 2017 baada ya kushindwa katika uchaguzi.
Gazeti la the Point, ambako Hydara alikuwa akifanya kazi kablaya kuuawa mnamo 2004, limeangazia kwamba imechukua miaka 15 kutambua nani aliyemuua mwandishi huyo.
Katika mtandao wake, gazeti hilo limeweka bango tangu wakati huo lililoambatana na swali, "Ni nani aliyemuua Deyda Hydara?".
Gazeti hilo halikutoa tamko jingine kuhusu taarifa hii ya sasa. Hydara aliwahi pia kulifanyia kazi shirika la habari la AFP na waandishi wasiokuwa na mipaka.
- ''Nilibakwa na rais wa zamani''
- Mali ya Yahya Jammeh kuuzwa kupitia mtandao
- Jammeh: Nitarudi Gambia kufanya ukulima
Kukiri kwa Luteni Jatta kunawiana na matokeo ya wanaharakati wa haki za binaadamu kama Human Rights Watch.
Ripoti yake imesema wahamiaji wa Afrika magharibi waliokiuwa wanaeleeka Ulaya walikamatwa na kuuawa baada ya boti walilokuwa wamepanda nchini Senegal kuishia nchini Gambia.
Yahya Jammeh ni nani?
- Aliingia madarakani kupitia mapinduzi mnamo 1994 akiwa na miaka 29
- Mnamo 2013, aliapa kusalia madarakani kwa "mabilioni ya miaka" Mungu akipenda
- Aliamuru mauaji ya wahalifu na wanasiasa wa upinzani walio kwenye hukumu ya kifo
- Alidai mnamo 2007 kwamba ana tiba ya ukimwi na ugumba kwa kutumia dawa za miti shamba
- Alionya 2008 kwamba wapenzi wa jinsia moja watakatwa vichwa
- Amekana kuwa maajeni wa usalama walimuua mwandishi Deyda Hydara mnamo 2004
- Atimuliwa madarakani mnamo January 2017 kupitia nguvu za kieneo baada ya kushindwa katika uchaguzi 2016
- Anaishi uhamishoni nchini Guinea ya Ikweta
Mwandishi wa Sierra Leone- na Gambian Ade Daramy anasema raia wa Gambia wanajaribu kupokea maovu yaliotekelezwa wakati wa utawala uliokuwepo.
Lakini anaeleza kwamba kuna kitu ambacho kinawaondolea raia hao wa Gambia tabasamu, vikao vya tume hiyo ya ukweli na maridhiano (TRRC).
Tume ya TRRC iliundwa kubaini "Rekodi ya historia ya hali, sababu na kiwango cha ukiukaji wa haki za binaadamu uliotekelezwa katika kipindi chaJulai 1994 hadi Januari 2017" - kipindi maalum kinachojumuisha utawala wa miaka 22 wa kiongozi huyo aliye uhamishoni sasa.
Daramy anafichua kwamba kilichobainika kutoka kwenye kikao hicho na kinachoendelea kuficguka ni kuchambuliwa gamba la maovu na muamko usiovutia vile kwa tiafa - unaolilazimu kujitathmini kwa mtazamo mpya na pengine mkali.
No comments:
Post a Comment