Adbox

Wednesday, July 24, 2019

Mohamed Salah Aingia Nairobi

Mohamed Salah: Mchezaji wa Liverpool atua Kenya

Mo SalahHaki miliki ya picha
Kumekuwa na msisimko Kenya kufuatia taarifa kwamba Mohamed Salah mchezaji nyota wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, yupo nchini Kenya.
Kwa mujibu wa Gazeti la Standard, Mohamed Salah aliwasili Kenya jana Jumanne jioni na kuondoka leo Jumatano asubuhi mwendo wa saa moja.
Picha za mchezaji huyo zimechipuka katika mitandao ya kijamii hii leo zikimuonyesha akiwa katika mojawapo ya hoteli za kifahari mjini Nairobi.
"Ndio. Salah alikuwa hapa. Aliwasili Jumanne jioni na kuondoka mapema leo asubuhi. Alikuwa katikati ya safari yake," afisa mmoja amenukuliwa na jarida la Game Yetu.
Wakenya katika mitandao ya kijamii hawakuweza kuizuia furaha yao kutokana na kusikia kuwa mchezaji huyo nyota yuypo nyumbani.
Baadhi wakichukua fursa kumkaribisha:
Wengine wakitamani japo kumuona kama @hamooy_gacal, aliyeandika katika twitter na kuomba ujumbe wake usambazwe hadi umfikie mchezaji huyo nyota wa Liverpool, 'Nataka kukuona @MoSalah
Nipo Nairobi, tafadhali nitafute'.
Swali ambalo baadhi wameishi kuuliza baada ya taarifa kuwa mchezaji huyo keshaondoka, ni kwanini kuingia na kuondoka ghafla?
Mshambuliaji huyo wa Misri na klabu ya Liverpool ndiye mchezaji bora wa mwaka wa shirikisho la Soka Barani Afrika kwa mwaka 2018 - ikiwa ni mara yake ya pili kushinda tuzo hiyo.
Salah, mwenye umri wa miaka 27, alimshinda mwenzake wa Liverpool Sadio Mane kutoka Senegal na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang kuwani atuzo hiyo.
Salah pia alitawazwa Mwanakandanda Bora wa Mwaka wa Afrika wa BBC kwa mara ya pili mtawalia Desemba.
Aliwafungia Liverpool mabao 44 msimu wa 2017-18 na kuisaidia klabu hiyo kufika fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ingawa walishindwa na Real Madrid.

No comments:

Post a Comment

Adbox