Korea Kaskazini imeilaumu Marekani kwa kuendeleza "uhasama", licha ya nchi hizo mbili kukubaliana kurejelea mazungumzo ya nuklia siku chache zilizopita.
Maafisa wa Pyongyang wametangaza kuwa Marekani bado ina mtizamo hasi dhidi ya taifa lao licha ya mkutano wa kihistoria wa hivi punde kati ya Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un.
- Shambulio la wahamiaji Libya ni uhalifu wa kivita?
- Tamasha la Nicki Minaj lazua gumzo Saudia
- Trump akutana na Kim kwenye mkutano wa kihistoria
Wawakilishi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa wamesema Marekani inataka kuhujumu mazingira ya amani yaliyoko katika rasi ya Korea na kuzitaka nchi zote kuwa waangalifu.
Pyonyang pia imeilaumu Washington kwa "kuhujumu hali ya amani inayoshuhudiwa" katika rasi ya Korea.
Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumapili alikutana na na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong-un katika eneo lisilokuwa na wanajeshi linalogawanya Korea Mbili.
Trump alikuwa rais wa kwanza wa Marekani aliye mamlkani kukanyaga Korea Kaskazini, na baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa saa moja wawili hao walikubaliana tena kurejelea mazungumzo ya nyuklia yaliokwama.
Lakini taarifa iliyotolewa na Korea Kaskazini siku ya Jumatano inaashiria mataifa hayo mawili huenda yakaanza tena kurushina cheche za maneno kama ilivyoshuhudiwa siku za hivi karibuni.
Kaorea Kaskazini imesema nini?
Ujumbe wa Korea Kaskazini umesema unajibu madai yaliotolewa na Marekani kuwa taifa hilo lilikiuka sheria inayoangazia uingizajiwa bidhaa za petroli kutoka nje iliyowekwa mwaka 2017.
Pia ilisema nchi hiyo imesema kuwa inajibu barua ya pamoja iliyotumwa na Marekani, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza kwa nchi wanachama wote wa Umoja wa Mataifa ambayo ilitoa wito Korea Kaskazini kuwekewa vikwazo zaidi.
Inaripotiwa kuwa barua hiyo ilyataika mataifa wanachama wa Umoja huo kuwafurusha wafanyikazi wa Korea Kaskazini kutoka nchini mwao.
"Kile ambacho hatuwezi kulifumbia macho ni ukweli kwamba barua hiyo ya pamoja iliandikwa .. siku ambayo rais Trump alipendekeza tupange mkutano mwingine," taarifa hiyo ilisoma.
"[Ina] zungumzia ukweli ulipo kuhusu mchezo unaoendelezwa na Marekani kuhusiana na suala la nyuklia na kwamba taifa hilo bado lina uhasama dhidi Korea Kaskazini ."
"Mataifa yote wanachama wa Umoja wa Mataifa yatalazimika kuwa macho kupinga jaribio la Marekani la kuhujumu hali ya amani inayoendela kushamiri katika rasi ya Korea," ilisema.
Pyongyang imeongeza kuwa ni "ajabu" Marekani inaonelea vikwazo kama njia pekee ya kutatua "matatizo yote".
Marekani hata hiyo haijatoa tamko lolote kuhusiana na taarifa hiyo.
Uhusiano wa Marekani na Korea Kaskazini ukoje?
Mazungumzo na Korea Kaskazini kujaribu kuishawishi kuachana na mradi wa nyukilia ambao ulifikia kilele mwaka jana wakati Trump na Kim walipokutana nchini Singapore.
Kwa pamoja waliahidi kuachana na mpango wa kutengeneza silaha za nyukilia, lakini bila kufafanua walimaanisha nini?
Kulikuwa na matumaini kuwa mkutanno wa Hanoi mwezi Februari ungewafanya viongozi hao wafikie makubaliano ya Korea Kaskazini kuachana na mradi wa nyukilia ili kuondolewa vikwazo.
Lakini mazungumzo hayo hayakuwafanya kufikia makubaliano yoyote, kwa kuwa walishindwa kukubaliana kwa amani kuhusu vikwazo vipi vingepatiwa unafuu.
Tangu kukwama kwa mazungumzo, rais Trump na Kim hivi karibuni wamekuwa wakiwasiliana kwa barua.
No comments:
Post a Comment