Adbox

Wednesday, July 3, 2019

Jaguar aachiwa kwa dhamana



Mbunge wa Jimbo la Starehe nchini Kenya, Charles Njaguar Kanyi maarufu Jaguar aliyekuwa anashikiliwa polisi kwa kauli yake iliyotafsiriwa na mamlaka kuwa ni ya kichochezi dhidi ya raia wa kigeni waishio Kenya kibiashara, ameachiwa huru kwa dhamana.

Jaguar ameachiwa kwa dhamana ya Laki tano za Kenya ni sawa na zaidi ya Shilingi Milioni 10 za Kitanzania.

Jaguar alipandishwa kizimbani kwa mara ya pili hii leo.

Ikumbukwe June 26, 2019 Mbunge huyo alikamtwa nje ya majengo ya Bunge kufuatia kauli zake za ‘kibaguzi' akiwataka wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wanaoendesha shughuli zao katika masoko mjini Nairobi na miji mingineyo kuondoka nchini humo ndani ya saa 24.

No comments:

Post a Comment

Adbox