Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia Erick Kabendera (39) mkazi wa Mbweni, Mwandishi wa habari, kwa mahojiano.
July 29, 2019 mtuhumiwa alikamatwa nyumbani kwake na Jeshi la Polisi baada ya kukataa wito wa Jeshi la Polisi.
Aidha mwandishi huyo awali aliandikiwa barua ya wito kufika Polisi kwa ajili ya mahojiano lakini alikaidi wito huo.
Ndugu waandishi wa habari niseme utii wa sheria bila shuruti ni muhimu sana kuzingatiwa kwani ukishindwa kutii sheria inakuwa shuruti.
Baada ya kukamatwa mwandishi huyo tumesikia taarifa mbalimbali zikisambaa kuwa mwandishi huyo ametekwa, niseme kuwa mwandishi huyo hajatekwa ila tumemkamata kwa mahojiano.
Aidha mtuhumiwa huyo kuna mashaka makubwa kuhusiana na uraia wake tutakapobaini mara moja tutamkabidhi kwenye idara ya uhamiaji ili kushughulika naye na ndiyo maana alikuwa akikaidi wito wa polisi na kujihami kuwa ametekwa.


No comments:
Post a Comment