Adbox

Monday, July 8, 2019

Iran kurutubisha urani na kukiuka makubaliano ya nyuklia


Hali ya wasiwasi ikiwa inaongezeka, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekosoa uamuzi huo wa Iran na kusema kwamba unakiuka makubaliano hayo ya nyuklia ambayo Marekani iliamua kujiondoa mwaka uliopita.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema hatua hiyo ni ya hatari sana na amezitaka nchi za Ulaya kuiadhibu Iran kwa kuiwekea vikwazo.
Katika mkutano na wanahabari, maafisa wakuu wa serikali ya Iran wamesema kuwa Iran itaendelea kupunguza uzingatiaji wake wa mkataba huo baada ya kila siku 60 iwapo mataifa yaliotia saini mkataba huo hayatachukuwa hatua za kuilinda dhidi ya vikwazo vya Rais wa Marekani Donald Trump.
"Tumejitayarisha kikamilifu kurutubisha madini ya urani kwa kiasi chochote kile," amesema Behrouz Kamalvandi, msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki Iran.

No comments:

Post a Comment

Adbox