Adbox

Monday, July 8, 2019

Macron amuonya Rouhani kwa madhara ya kuodhoofisha makubalino ya nyuklia

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amemuonya mwenzake wa Iran Hassan Rouhani, kwamba ana wasiwasi mkubwa kuhusu kuendelea kudhoofishwa zaidi mkataba wa nyuklia wa Iran uliofikiwa mwaka 2015 na kuonya kuCwa madhara yatafuata
Macron, ambae alizungumza na rais wa Iran Rouhani, siku moja kabla ya Iran kujiandaa kuongeza urutubishaji wa madini ya urani kupita kiwango kilichowekwa katika makubalino yake na mataifa makubwa, amesema anataka kuweka msukumo wa kufanyika mazungumzo kuanzia sasa na Julai 15, kwa lengo la kuzirudisha pande zote katika meza za mazungumzo.
Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais wa Ufaransa Macron amesema " rais ameonesha wasiwasi mkubwa, kutokana na hatari viashiria vya udhoofishiji wa mkataba wa nyukilia wa mwaka 2015, madhara ambayo yatakufuata" Lakini haijawa wazi kwamba madhara gani hasa ambayo taarifa hiyo inayazungumzia. Hata hivyo maafisa katika ofisi ya Macron, hawakuweza kupatikana kutoa ufafanuzi wa hoja hiyo.

Rais Hassan Rouhani wa Iran


Mkwamo wa utekelezaji wa mkataba

Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya wamesema kuendelea kukiukwa zaidi kwa mkataba huo, kunaweza kusababisha upande wa Ulaya yaani Ufaransa, Uingereza na Ujerumani kukawepo kwa mtibuano wa muundo wa maazimio ndani ya mkataba wenyewe, jambo ambalo linaweza kuchangia kuzushwa kwa uwekwaji wa vikazo vya Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment

Adbox