Aliyekuwa mkurugenzi wa mawasiliano ya kidijitali katika ikulu nchini Kenya Dennis Itumbi amezuiwa na polisi kuhojiwa kuhusu barua ya njama ya kumuua naibu rais William Ruto.
Itumbi amekamatwa na wapelelezi wanaochunguza tuhuma za njama ya kumuua naibu rais William Ruto.
Anazuiwa katika makao makuu ya idara ya upelelezi mjini Nairobi, linaripoti gazeti la The Standard.
- Mawaziri nchini Kenya wakana kupanga njama za kumuua Ruto
- Rais Kenyatta amwandikia Magufuli kuhusu kauli ya Jaguar
Anakamatwa siku kadhaa baada ya taarifa kwamba chanzo cha barua hiyo ghushi kimetambulika - barua iliyozusha tuhuma za kutaka kuuawa Ruto.
Wiki iliyopita, mawaziri kadhaa nchini Kenya walikana kupanga njama za kumuua Naibu Rais William Ruto.
Waziri wa biashara wa Kenya Peter Munya amekana shutuma za kupanga mauaji ya Naibu Rais William Ruto, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.
Waziri Munya alikuwa akizungumza nje ya makao makuu ya ofisi ya Mkurugenzi wa uchunguzi wa makosa ya jinai (DCI) ambako aliitwa , sambamba na mawaziri wengine, kuhojiwa kuhusu shutuma kuwa walimtishia bwana Ruto, Gazeti la the Standard limeripoti.
No comments:
Post a Comment