Adbox

Sunday, May 10, 2020

Madagascar yaendelea kugawa dawa ya Corona licha ya kuwepo shaka na upinzani

Licha ya kuwepo shaka na upinzani dhidi ya dawa inayodaiwa kutibu ugonjwa wa Covid-19, serikali ya Madagascar inaendelea kugawa dawa hiyo.

Kanali ya televisheni ya France 24 imeripoti kwamba pamoja na wasi wasi wa jamii ya kimataifa kuhusiana na taathira na matokeo ya dawa hiyo ya ya Covid Organics iliyotengenezwa na Madagascar, lakini viongozi wa nchi hiyo wameanza kuisambaza kwa nchi za Afrika kwa lengo la kutibu ugonjwa wa Covid-19.


 Dawa hiyo iliyoandaliwa kutokana na mti unaoitwa Artemisia, imegawiwa kwa kiasi kikubwa nchini humo. Kwa mujibu wa kanali hiyo ya France 24, katika hali ambayo dawa hiyo ambayo ni aina ya kinywaji bado haijafanyiwa utafiti wowote wa kielimu, lakini imeidhinishwa na Rais Andry Rajoelina wa Madagascar na kuanza kusafirishwa katika nchi

Alkhamisi iliyopita, Shirika la Afya Duniani sambamba na kutahadharisha juu ya matumizi ya dawa ya Covid Organics, liliwataka viongozi wa serikali ya Antananarivo kuifanyia utafiti wa kitiba. Aidha Umoja wa Afrika umeitaka Madagascar kuweka wazi matokeo ya uchunguzi wa kitaalamu kuhusiana na taathira na usalama wa dawa hiyo.

 Hata hivyo, nchi za Afrika zikiwemo Niger, Equatorial Guinea, Senegal, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania tayari zimekwishaagiza dawa hiyo kwa ajili ya kuifanyia utafiti. Licha ya Madagascar kusajili kesi 193 za waathirika wa virusi vya Corona, lakini hakuna mtu yeyote nchini humo aliyethibitishwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

No comments:

Post a Comment

Adbox