Kauli hiyo ameitoa jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisni kwake kuhusu hali ya mwenendo wa mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Mhandisi Kamwele amesema kuwa meneja wote wa TANRODS nchini wahakikishe wanaimarisha ukaguzi wa miundombinu ya barabara na madaraja katika maeneo yao ili pasitoke barabara kuu au ya mkoa yoyote kufungwa.
Aidha Mhandisi Kamwele amesema kuwa kama alivyo elekeza Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa meneja wa TANROADS ambaye barabara zake zitakatika naye atakuwa amejifuta kazi.
“Nasisitiza kuwa sitakuwa na mzaa katika utekelezaji wa maelekezo hayo”, amesisitiza Mhandisi Kamwele.
Hata hivyo ameongeza kuwa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini wahakikishe wanatoa taarfa ya hali ya hewa hususani za mvua mara kwa mara kwa wananchi ili waweze kuchukua tahadhali juu ya taarifa watakayo kuwa wamepatiwa na watalamu wa hali ya hewa.
Waziri Kamwele ametoa wito kwa wananchi wote kuchukua tahadhali ikiwemo kuzingatia taarifa zinazo tolewa na Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania sambamba na kutafuta na kufuata ushauri unao tolewa na sekta husika ili kupunguza athari mbaya zinazotokana na hali ya hewa na mabadiliko ya tabia ya nchi.


No comments:
Post a Comment