Mkutano huo uliokuwa uwakutanishe viongozi wa mataifa ya Canada, Ufaransa, Ujerumani, Japan, Italia, Uingereza na Marekani ulikuwa ufanyike mnamo mwezi Juni katika jimbo la Marekani la Maryland.
Trump pia atakutana na viongozi wa mataifa hayo saba kwa njia ya video mnamo mwezi Aprili na Mei baada ya viongozi hao kufanya mkutano kuhusu mripuko wa virusi vya corona wiki hii.
Kwa hali inavyoendelea, serikali ya Trump inaamini mripuko wa virusi vya corona utaendelea kuwa na athari ulimwenguni hadi majira ya joto.


No comments:
Post a Comment