Mataifa thelathini na sita kati ya 54 hadi sasa yamesharipoti maambukizi ya virusi hivyo ambayo jumla yake ni 720.
Hapo jana Chad na Niger zilitangaza kuthibitisha maambukizi yake ya kwanza.
Na kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya corona kikiwa kimeripotiwa wiki tatu zilizopita katika mataifa yaliyo kusini mwa jangwa la Sahara.
Mataifa mengine zaidi barani humo yametangaza kufunga mipaka yake kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo katika bara lenye idadi ya watu wapatao bilioni 1.3.
Moeti amesema haamini kwamba idadi kubwa ya walioambukizwa barani humo wameshindwa kutambuliwa lakini amekubali kwamba kuna upungufu wa vifaa vya kufanyia vipimo vya virusi hivyo vya corona.


No comments:
Post a Comment