Adbox

Tuesday, March 3, 2020

Uturuki yakataa msaada wa dollar bilioni 1,1 kutoka Umoja wa Ulaya

Rais Erdoğan asema kuwa Uturuki haina haja ya pesa zilizoahidiwa na Umoja wa Ulaya  kwa ajili ya kuhudumia wakimbizi.

Katika mkutano na waandishi wa habari, rais Erdoğan amezungumza  ahadi isiotekelezwa iliotolewa na Umoja wa Ulaya kuhusu  mahitaji ya wakimbizi.

"Ni mara  kadhaa  wamesema kuwa watatuma pesa kwa aji ya kukidhi mahitaji ya wakimbizi, ni nani ambae  mnajaribu kumdanganya? hatuna haja ya pesa hiyo" amesema rais Erdoğan.

Mkutano huo na waandishi wa habari umefanyika  Jumatatu.

Rais Erdoğan amesema kuwa Uturuki haina haja ya dola bilioni 1,1 ambazo  Umoja wa Ulaya umefahamisha kuwa zitatumiwa kwa ajili ya  kukidhi mahitaji ya wahamiaji na wakimbizi kutoka Syria na mataifa mengine  zaidi  ya milioni  nne waliopo Uturuki.

Rais Erdoğan amezungumza na waziri mkuu wa Bulgaria Boyko Borisov katika ziara yake nchini Uturuki.

No comments:

Post a Comment

Adbox