Adbox

Tuesday, March 3, 2020

Serikali kutoa elimu juu ya Udhibiti Upotevu wa Chakula Shambani

Na John Walter, Manyara

Serikali imeanza mpango mkakati wa kuunda majukwaa ya kilimo katika halmashari zote nchini ili kukabiliana na upotevu wa mazao shambani kipindi cha uvunaji.

Akizungumza katika kikao cha wadau wa kilimo katika Halmashauri ya Mji wa Babati Afisa kilimo mkuu kutoka wizara ya kilimo idara ya usalama  wa chakula Bi Magreth Natai, amesema lengo la mkutano huu nikutoa elimu kwa wadau wa kilimo pamoja na kuunda majukwa ya wadau ili kupunguza upotevu wa chakula.

Aidha amesema mpaka sasa mikoa mitano kutoka kanda ya ziwa ambayo ni Mkoa Mwanza shinyanga Simiyu Geita na Mkoa wa Mara tayari imefikiwa na kuweza kuunda majukwa ya wadau wa kilimo na kwa awamu ya pili wanaendelea na Mkoa wa Manyara,Morogoro na Dodoma.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Babati Fortunatus Fwema awali akifunguwa kikao hicho amesema kumekuwa na upotevu mkubwa wa mazao hasa kipindi cha upandaji mpaka uvunaji hivyo serkali kwakulitambuwa hilo limeanza kutekeleza mpango Mkakati utakaodhibiti hali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Adbox