Hata hivyo Waziri amesema kuwa daraja hilo kwa sasa halitapitisha magari mawili kwa pamoja badala yake gari moja tu litaruhusiwa kupita hadi hapo utaratibu mwingine utatakapotolewa.
Aidha, Waziri amesema karavati la awali ambalo limevunjika lilikuwa na kipenyo cha Mita tatu tu na sasa yamewekwa makaravati mawili kila moja likiwa na kipenyo cha Mita tatu hivyo kuruhusu maji mengi kupita kwa wakati mmoja tofauti na awali.
Akitoa matumaini kwa watanzania hususana madereva wanaotumia barabara hiyo ya Morogoro – Dodoma, Waziri amesema kazi ya kujenga daraja la kudumu katika eneo hilo utafanyika mara baada ya mvua kupungua.
Kwa upande waka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amewashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha tangu adha hiyo ilipotokea hususan madereva kwa kutii maelekezo ya Serikali walipotakiwa kubaki maeneo waliyokuwapo hadi watakapoelekezwa vingine.
Daraja la Mto Mkange lililopo katika Kijiji cha Kiegeya Wilayani Kilosa lilivunjika Machi 2 Mwaka huu majira ya saa kumi jioni kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hapa nchini na kusababisha adha kubwa kwa wasafiri na Usafirishaji.


No comments:
Post a Comment