Hayo yameelezwa na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mahamoud Thabit Kombo katika Ukumbi wa ZSSF Kariakoo katika ghafla ya utiaji saini kuhusu Ushirikiano wa Utendaji wa mambo yasiyo ya Muungano katika Wizara zenye dhamana ya mambo ya habari.
Alisema makubaliano hayo yatasaidia katika matumizi ya ndege zisizo na rubani na upatikanaji wa chanali ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) katika ving’amuzi vyote nchini bila ya malipo kwa lengo la kuimarisha uhusiano na kukuza lugha ya hiyo Nchini.
Alifahamisha kuwa makubaliano hayo pia yataendeleza ukuaji wa Kiswahili kimataifa kwa kutoa waandishi wa habari kutoka Tanzania amabao watatumia na kukitangaza Kiswahili katika vyombo hivyo pamoja na uanzishwaji wa vituo vya utamaduni nje ya nchi.
Waziri Kombo alieleza kuwa wataendeleza kutangaza utalii na utamaduni nje ya nchi na kuimarisha michezo pamoja na kukuza utendaji kwa lengo la kuleta maendeleo nchini.
Aidha Waziri Mahamoud alifahamisha kuwa jukumu la kufundisha na lugha ya Kiswahili nchini ni Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) na baraza la Kiswahili la Tanzania (BAKITA) hivyo ni vyema kutoa wataalamu wazuri wataofundisha lugha hiyo ili iweze kukua na kuimarika zaidi.
“Inashangaza sana kumkuta mtu asie Mtanazania anafundisha Kiswahili nje ya nchi au waajiriwa wasio Watanzania wanaajiriwa kwa kigezo cha lugha ya Kiswahili,mfano wa wazi ni shirika l ndege la kimataifa la Emirates Airline waajiriwa wengi walioajiriwa kwa minajili ya kutumia Kiswahili ni Wakenya na sio Watanzani ni jambo la kushangaza” alisema Waziri Mahamoud.
Kwa upande wake Waziri wa habari wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania Dkt Harrison Mwakyembe amesikitishwa na baadhi ya raia wasio Watanzania kutumia njia hiyo ya kutumia lugha ya kiswahili ili kupata ajira bila ya watanzania wenyewe kufaidika nayo .
Nae Waziri wa Vijana Sanaa Utamaduni na Michezo Balozi Ali Karume alisema mashirikano hayo yana umuhimu mkubwa kwani yatapelekea kubadilishana na kupanua wigo katika kuleta maendeleo katika sekta ya habari na Utamaduni lengo la kuimarisha utendaji.
Balozi Ali Karume amefahamisha kuwa katika mambo ya michezo ni lazima kushirikiana kwa pamoja katika kufanya shughuli zao ikiwemo Kombe la M apinduzi ili kukuza lugha ya Kiswahili wakati watakapokwenda kufanya mashindano nje ya Tanzania.


No comments:
Post a Comment