Serikali ulimwenguni kote hivi sasa zimegeukia teknolojia kupambana na virusi hivyo. App hiyo inayoitwa TraceTogether itakuwa inabadilishana taarifa za watu wanaopishana kwa umbali usiozidi mita 2 kupitia bluetooth ili kutambua taarifa za mtu mwingine.
Rekodi zao zitatunzwa kwenye app iliyoko kwenye simu. App hiyo imetengenezwa na shirika la teknolojia la serikali ya Singapore la GovTech kwa kushirikiana na wizara ya afya.
Ingawa hakuna atakayelazimishwa kuwa na app hiyo lakini serikali imesema itawahamasisha kuwa nayo.


No comments:
Post a Comment