Adbox

Thursday, March 12, 2020

Serikali tunatekeleza mikataba ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia

Na Timothy Itembe Mara.

SERIKALI imesema kuwa inatekeleza mikataba ya kimataifa iliyosaini juu ya kupinga ukatili wa kijinsia na kuwa wale ambao wanafanya tohara kwa vijana wa kiume na wanaume kwa ujumla wanatakiwa kutambuliwa huku wakielimishwa juu ya  kufanya toharasalama ikiwemo na kupimwa Afya zao.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa wilaya Tarime Mtemi Msafiri mbele ya Baraza la madiwani wa halmashauri ya Tarime vijijini lilioloketi Nyamwaga la kujadili utekelezaji wa shuguli za maendeleo kwa wananchi wake.

Msafiri alisema kuwa wao kama serikali wanasimamia utekelezaji wa mikataba ya kimataifa iliyosainiwa na Serikali ya Tanzania inayopinga ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji wa mtoto wa kike kuwa kufanya hivyo nikukiuka mikataba tuliyosaini na kuwa serikali itawashugulikia wale wote ambao wanajihusisha na vitendo vya kuwakeketa watoto wa kike.

"Nikosa kumkekketa mtoto wa kike na hili liko kwenye sheria na tumeridhia mikataba ya kimataifa inayopinga ukatili wa kinisia na hili la kumkeketa mtoto wa kike ni ukatili linatakiwa kutokomezwa licha ya kuwa kuna baadhi ya mila zinashabikia kuwepo vitendo hivyo kwa baadhi ya jamii"alisema Msafiri.

Mkuu wa wilaya huyo aliwataka pia madiwani kusimamia shuguli za utekelezaji wamiradi kwa jamii inayokuwa inatekelezwa ndani ya kata zao huku wakipinga na kufichua wale wote ambao wanatumia nafasi zao kupokea na kutoa Rushwa kitendo ambacho  nikikwazo cha maendeleo.

Msafiri alitumia nafasi hiyo kuwataka wanawake kuijitokeza kwa wingi kuchukua famo za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika maeneo yao na kuwatakia wale ambao wako kwenye nafasi ya udiwani kipiondi hiki kugombea na kutetea nafasi zao zaudiwani katika kata zao.

Mkuu huyo aliongeza kusema kuwa kama serikali itashugulika na wale wote ambao wanatekeleza vitendo hivyo kinyume cha sheria ikiwa ni pamoja na kuwakamata na kwa wale ambao wanafanya Tohara kwa wanaume wanatakiwa kutambuliwa na kupewa elimu ya tohara salama huku wakipimwa Afya zao.

Naye diwani wa Mbogi mchugaji Kibaki Kibaki alitumia nafasi hiyo kuitaka halmashauri hiyo kumpatia mwalimu wa kike katika shule ya sekondari ya Mbogi ili kusaidia wanafunzi wa kike waliopo shuleni hapo kwa maswala mbalimbali yanayojitokeza huku akitatua changamoto zinazowapata wanafunzi wa kike.

Shule yangu ya Sekondari Mbogi haina mwalimu wa kike hata moja kwa hali hiyo nilitumia siku ya wanawake duniani kutoa kilio changu mbele ya wananchi waliohuidhuria maadhimisho yao ambapo niliomba halmashauri ya Tarime vijijini kupitia mkurtugenzi wake Apoll Tindwa kuniletea   mwalimu wa kike katika shule hiyo ili kuja kusaidia wanafunzi wa kike walipo aliongeza kusema Kiobaki.

Kwa upande wake kaimu mkiurugenzi wa halmashauri ya Tarime Vijijini,Sylvanus Gwiboha alisema kuwa halmashauri yake inatekeleza utekelezaji wa mikataba ya serikali iliyosaini juu ya kupinga ukatili wa kijinsia.

No comments:

Post a Comment

Adbox