Rais Cyrill Ramaphosa ametangaza siku 21 za wananchi wote kujifungia ndani ilikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya #COVID19 nchini humo
Rais Ramaphosa amesema wakati wa utekelezaji wa suala hilo linalotarajia kumalizika Aprili 16 hakuna mtu ataruhusiwa kutoka nyumbani na watakosimamia jambo hilo ni idara ya Maafa ya nchi hiyoKatazo hilo la watu kutoka ndani halitawahusu watu wa Idara ya Majanga, Polisi na Watumishi wa Afya watakaokuwa wakizunguka kwa wananchi kuwapatia mahitaji muhimu pamoja na chakulaHadi leo asubuhi, Nchi hiyo imeripoti jumla ya Maambukizi 402 huku kukiwa na Wagonjwa wanne waliopona
No comments:
Post a Comment