“Naishukuru sana Serikali ya Ujerumani kwa kufadhili ujenzi wa karakana hii ya kisasa ya matengenezo ya magari na mafunzo ya ufundi ya JWTZ, nawashukuru pia Ujerumani kwa misaada na ushirikiano mkubwa wanaoendelea kutoa kwa Nchi yetu katika sekta mbalimbali”- JPM
“Nitoe wito kwa JWTZ kutumia vizuri karakana hii, vitunzeni vifaa ambavyo tumekabidhiwa na Serikali ya Ujerumani na ambavyo vitaendelea kuja, muhimu zaidi hakikisheni mnatumia vizuri karakana ili iwe chachu ya kuwaimarisha kiufundi na kuchochea maendeleo“-JPM
“Karakana hii itatumika kutengeneza magari yetu ya kijeshi na pia kutoa mafunzo kwa mafundi, hii itasaidia kupunguza gharama kwa jeshi letu pamoja na kuwaongezea uwezo wa kiufundi wanajeshi wetu”-JPM

No comments:
Post a Comment