Adbox

Saturday, March 14, 2020

Breaking News: Kisa cha kwanza cha virusi vya Corona chathibitishwa Rwanda

Raia wa India aliyewasili nchini humo kutoka Mumbai, India, Machi 8, 2020 amethibitishwa kuwa na virusi vya corona.

Kulingana na wizara ya afya, mgonjwa huyo hakuwa na dalili zozote za virusi vya Corona wakati anawasili nchini Rwanda na alijipeleka mwenyewe kwenye kituo cha afya Machi 13, ambapo alifanyiwa vipimo mara moja.

Kwa sasa anaendelea na matibabu, hali yake imeimarika na ametengwa na wagonjwa wengine.

Wote aliotangamana na mgonjwa huyo wanaendelea kutafutwa katika juhudi za kuudhibiti ugonjwa huo.

Raia wote wa Rwanda wanastahili kufuata sheria zote zilizotolewa na wizara ya afya hasa kuhusu kuosha mikono kila mara, kuepuka mikusanyiko mikubwa na kuripoti dalili zozote kwa kupiga simu kwa nambari iliyotolewa na wizara hiyo bila malipo.

Aidha, shirika la ndege la Rwanda limetangaza kusitisha safari zake za ndege kwa muda kwena nchini India kwasababu ya mlipuko wa Corona hadi Aprili 30, 2020 na kuahidi kwamba aitachukua hatua kadhaa kwa safariki walioathirika kama kubadilisha safari zao bila malipo ya ziada au hata kuwarejeshea pesa zao walioathirika.

Wakati huohuo, Sudan imesema mwanamume aliyekuwa na umri wa miaka ya 50 na kuaga dunia Alhamisi katika mji mkuu wa Khartoum alikuwa na virusi vya Corona.

Mwanamume huyo alikuwa ametembelea Falme za Kiarabu wiki ya kwanza ya mwezi Machi, kwa mujibu wa mamlaka.

Sudan imesitisha utoaji wa visa kwa nchi 8 ikiwemo Italia na nchi jirani ya Misri kwa hofu ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

Nchini Misri, usafiri wa basi pia umesitishwa.

Misri ilikuwa nchi ya kwanza Afrika kuthibitisha kisa cha kwanza cha virusi vya corona pamoja na vifo viwili vya ugonjwa huo huku visa 80 vikiripotiwa.

Aidha, kisa cha kwanza cha virusi vya corona kimethibitishwa nchini Kenya. Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema kwamba mtu mwenye maambikizi ya virusi vya Corona alithibitishwa kuwa ana maambukizi hayo Alhamisi usiku.

Nchini Ethiopia mamlaka za nchi hiyo pia imetangaza kisa cha kwanza cha maambukizi ya coronavirus. Mgonjwa wa Ethipia ni raia wa Japan.

No comments:

Post a Comment

Adbox