Adbox

Saturday, February 8, 2020

Wizara ya Elimu yaipa heshima kubwa shule ya Sekondari Komoto kwa kufanya vizuri kidato cha Nne

Na John Walter-Manyara

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kutambua juhudi za shule ya Sekondari Komoto iliopo Halmashauri ya mji wa Babati mkoa wa Manyara, imeipatia zawadi ya Kikombe kama pongezi kwa kufanya vizuri kwenye mtihani wa kidato cha nne mwaka 2018.

Shule hiyo ilishika nafasi ya kumi katika mkoa wa Manyara kwa matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne kati ya shule 115 wakati kitaifa imekuwa shule ya 523 kati ya shule 3,908 .

Shule ya Sekodari Komoto mwaka 2017 ilifaulisha wanafunzi kwa asilimia 77 huku mwaka 2018 ikiongeza ufaulu kwa asilimia 22 na kufikia asilimia 99 na haikuwa na wanafunzi waliofeli (division zero).

Akizungumza wakati wa kuwatunuku zawadi hiyo ya kikombe, mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Yona Wawo amessema kuwa matokeo hayo yameitia moyo halmashauri yake,hivyo motisha waliyoitoa Wizara inatoa hamasa kwa walimu na wanafunzi kujituma zaidi.

Amesema nafasi iliyoshika shule hiyo, halmashauri yake inatarajia kuona ikiwa kinara zaidi katika nchi kwenye viwango vya ufaulu na kuwataka waalimu na wanafunzi kuendelea kushirikiana ili kuinua kiwango cha ufaulu zaidi ya hapo.


Naye mkuu wa shule hiyo Mwalimu Dennis Bakuza amesema wameweza kufanikiwa hayo kwa kuwa walizibadili changamoto kuwa fursa na kuzitumia ipasavyo mbali na kuishia kulalamika huku pia akiahidi shule yake kuitoa halmashauri na mkoa kimasomaso katika matokeo ya kitato cha nne kitaifa.

Ikumbukwe kuwa shule ya Sekondari Komoto ilianzishwa mwaka 2010 kwa  kuanza na kidato cha kwanza hadi cha nne.

No comments:

Post a Comment

Adbox