Adbox

Saturday, February 22, 2020

Waziri Mkuu aagiza KUWASA kulipa deni wanalodaiwa na TANESCO

Na Theo Mwambasi George, Kigoma.

Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa ameitaka mamlaka ya maji safi na maji Taka Kigoma(KUWASA) kulipa deni inayodaiwa na shirika la umeme mkoani kigoma ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi wa mkoa huo.

Akizungumza katika mkutano  na wananchi wa mkoa wa Kigoma uliofanyika hapo jana jioni katika viwanja vya Mwanga community center Majaliwa amemtaka meneja wa TANESCO kutoa sababu kwanini wanakata umeme hali inayopelekea wananchi kukosa maji ndipo Meneja wa TANESCO Kigoma kudai kuwa wanaidai KUWASA deni ambalo mpaka sasa halijalipwa.

Hata hivyo waziri mkuu alichukua jukumu la kumuliza meneja wa KUWASA mbele ya wananchi ambapo meneja huyo amekili kuwepo kwa deni hilo ambalo ni Zaidi ya Tsh.millioni mianne(400,000,000) ambapo kwa maelezo ya meneja huyo alidai kuwa deni hilo ni la nyuma na kwasasa wanailipa billi ya umeme TANESCO bila shida.

Aidha kwa maelezo hayo ndipo waziri mkuu Majaliwa akasema haiwezekani kulipa billi ya sasa wakati kuna deni la nyuma linadaiwa ,hivyo akamtaka meneja wa KUWASA kuanzia juma tatu 24 february waanze kulipa deni la nyuma ili kusiwepo tena changamoto ya wananchi kukosa maji katika mitaa yao.

Mbali na hilo Waziri mkuu amesikitishwa na baadhi ya wananchi wa kigoma kwa kuwa na tabia ya ubinafsi katika suala la maendeleo katika mkoa wao na kuwataka kuacha hiyo tabia mara moja ambapo amesema wananchi wa kigoma wanazuia maendeleo yasifanyike hususani katika maeneo ambayo ujenzi wa huduma za kijamii unaweza fanyika.

Amesema kuna baadhi ya wananchi wamezuia maeneo yao usifanyike ujenzi wa hospital ya rufaa katika mkoa huo huku wakidai fidia ya eneo hilo licha ya kuwa eneo hilo ni pori na halina shughuli yoyoye ambapo pia ameeleza kuwa serikali imeshindwa kuongeza ukubwa wa kiwanja cha ndege mkoani humo kulingana na watu wanaomiliki ardhi zao kuwa wabishi kuachia maeneo hayo na kukwamisha maendeleo hivyo kuwa na changamoto kubwa ya kutofika kwa ndege kubwa kama AIR BUS katika uwanja wa ndege Kigoma.

Sanjari na hilo amemalizia kwa kutoa ufafanuzi kuwa serikali inamlipa mtu fidia kwa nyumba na shamba ambalo hasa mazao yamepandwa na kuwataka wananchi kuhakikisha wanamiliki ardhi kisheria.

No comments:

Post a Comment

Adbox