Adbox

Wednesday, February 12, 2020

Wananchi watakiwa kutunza miondombinu ya reli ya Tazara

Wananchi wanaoishi  katika maeneo yote inapopita   reli ya Tazara wametakiwa kutunza na kuheshimu  miondombinu ya hiyo na kuwafichua watu wanaoihujumu miundombinu ili iendelee kusaidia kuinua uchumi wa  Taifa.

Hayo yalisemwa na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Tazara, Kamishna  Msaidizi wa Polisi( ACP) Advera Bulimba wakati wa ziara ya kimafunzo  katika mitambo ya kuzalisha kokoto na mataruma ya reli kilichopo eneo la Kongoro jijini Mbeya.

Kamanda Bulimba  alisema kuwa kumekuwepo na tabia kwa baadhi ya wananchi kujihusisha  na vitendo vya uhalifu vya kung’oa na kuiba miundombinu ya reli kna kwenda kuuza kama vyuma chakavu jambo ambalo linadhoofisha  utendaji wa reli ya Tazara.

“Madhara ya kuhujumu reli ni makubwa  na yanaweza kugharimu maisha ya watu na kusababisha ulemavu wa kudumu, jambo hilo halitakubalika chini ya uongozi wa kikosi cha Polisi Tazara”  alisema  Kamanda Bulimba

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa  reli ya Tazara Fuad Abdala akiwa ziarani humo aliwataka wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha kokoto na mataruma ya reli kutumia vizuri na kuitunza mitambo hiyo iliyonunuliwa ili iweze kutumika kwa muda mrefu.

Aliwataka wafanyakazi  wa kiwanda hicho kuendelea kufanya kazi kwa kujituma na kutunza mitambo hiyo kwa kuwa kiwanda hicho ndiyo roho ya Tazara katika kuimarisha miundombinu ya reli.

Meneja Mkuu wa Tazara, Fuad Abdala alisema,  lengo la ziara hiyo ilikuwa kuangalia utekelezaji wa maazimio ya ziara ya mwezi Februari, mwaka jana na kuongeza kuwa ameridhishwa na utendaji kazi wa kiwanda hicho na kuahidi kuendelea kutatua changamoto za wafanyakazi na kiwanda kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Adbox