Hakimu Amy Berman Jackson, alitoa hukumu ya kifungo cha miaka 3 na miezi 4 kwa Stone.
Stone alikamatwa mwaka jana mwezi Januari, katika tuhuma ambazo zilikuwa zikihusu Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2016, uchunguzi wa tuhuma hizo uliendeshwa na mjumbe maalum, mwanasheria msomi Robert Mueller.
Katika hati ya mashitaka Stone alihusishwa na kuvuja kwa ujumbe wa barua pepe wa aliekuwa msimamizi mkuu wa kampeni wa mshindani wa Rais Trump katika uchaguzi mkuu wa Rais Bi Hillary Clinton. Ujumbe huo ulifika katika computa za maharamia wa mtandao wa kirusi na kishwa kusambazwa katika kurasa za mtandao za Wikileaks.


No comments:
Post a Comment