Adbox

Thursday, February 20, 2020

Mkuu wa Magereza Nchini akagua Ujenzi wa nyumba za maafisa, Gereza la Isanga Dodoma

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Mkuu wa Magereza Nchini, Kamishna Jenerali wa Magereza Suleimani Mzee, ametembelea miradi inayotekelezwa na Magereza Mkoa wa Dodoma ikiwamo mradi wa ufyatuaji tofali na Ujenzi wa nyumba 20 za kujitegemea za maafisa wa magereza.


Akiwa katika gereza la Isanga ambapo miradi hiyo inatekelezwa Kamishna Jenerali Suleimani Mzee amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Jeshi la Magereza Mkoa wa Dodoma akitaka na mikoa mingine kuiga mfano huo.

Akiongea na vyombo vya habari Mara baada ya kumaliza kukagua miradi hiyo, amesema ameamua kuwaleta wakuu wa Magereza nchi nzima kuiga mfano huo ili kila Mkoa ukatekeleze miradi kulingana na Jeografia yake.

" Tulikuwa na kikao na Wakuu wa Magereza nchi nzima hapa Dodoma, na katika kikao hicho nimesisitiza kuhakikisha kila gereza linajitegemea na kuwa na miradi ya kujiendesha, niwapongeze Dodoma kwa Ujenzi wa nyumba hizi nataka mikoa mingine muige"

"Sio kila Mkoa lazima mlime au mfuge kila Mkoa una Jeografia yake kila Mkoa uone katika Mkoa wake wataanzisha nini kitakachopelekea waweze kujitegemea" Amesema Kamishna Jenerali, Mzee.


Aidha amesisitiza  kuhakikisha kila Mkoa unabuni vitega uchumi kuhakikisha kila gereza linajitegemea kwa kila kitu bila kutegemea serikali kujiendesha kwa sababu rasilimali na nguvu kazi zipo sambamba na kusimamia rasilimali walizonazo ili ziweze kuzalisha.

Amesema Jeshi hilo linamiradi mingi kupitia shirika lake la Magereza ambalo linavitega uchumi vingi Kama Mashamba, mifugo ya aina mbalimbali na kila Mkoa kuna viongozi ambao wanasimamia na baadaye kuunganishwa katika shirika hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma Keneth Mwambije, amesema ujenzi wa nyumba hizo umetumia fedha kidogo ambapo ujenzi na kupaua wametumia milioni Saba (7)kwani kwa kiwango kikubwa wametumia nguvu kazi na rasilimali walizonazo.

No comments:

Post a Comment

Adbox