“Ni marufuku kuanzia sasa kutumia karatasi za daftari kuomba dawa kutoka idara moja kwenda nyingine, tuandae fomu maalum za maombi” Amesema Dkt. Ndugulile
Ameagiza kuwa dawa zote zinazopatikana katika vituo vya kutolea huduma ziwekwe kwenye fomu za maombi (reiquizitaion form) huku zikionyesha jina la aliyeomba pamoja na kusaini kuthibitisha maombi yake ya dawa.
Amesepa pia mtu au idara ya famasi inayopoke maombi hsyo anatakiwa kuhakikisha maombi hayo na kusaini fomu hiyo.
“Ni marufuku kwa mtu wa famasi kujiongezea dawa kwa maneno ya mdomo au kuambiana, na atakayepokea dawa hizo pia anatakiwa aandike jina lake na kusaini.
Hatua hiyo inakuja mara baada kubaini mianya ya upotevu wa dawa za Serikali ambapo Dkt. Ndugulile amesema “Serikali imewekeza nguvu kubwa sana katika upande wa dawa, lakini pia nyie wataalam ambao mnasimamia mnatakiwa kuhakikisha mnaweka kumbukumbu zenu sahihi ili kudhibiti mianya ya upotevu wa dawa”
“Hapa nnapata mashaka kuwa kuna uptevu wa dawa za Serikali tujirekebishe na kuhakikisha tunatunza vzuri kumbukumbu zetu” Amesema Dk. Ndugulile na kuwataka kuhakikisha wanaweka mifumo ya TEHAMA katika kusimamia maombi ya dawa.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (Mawenzi) Dkt. Jumanne Karia amesema wamepokea maelekezo hayo na kuahidi kuyatekeleza mara moja.
“Tunashuruku kwa maelekezo yako, tutaendelea kuunga mkono Wizara ya Afya na tutatekeleza maelekezo uliyoagiza” Amesema Dkt. Karia.


No comments:
Post a Comment