Agizo la Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani la kuitaka Kampuni ya SINOTEC Co Limited kuwasha umeme Kitongoji cha Chasimba Kata ya Yombo, linatekelezwa kwa kasi na Kampuni hiyo.
Meneja wa Kampuni hiyo Peter Jeremiah amemwambia Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa aliyeambatana na wa Viti Maalumu Zaynabu Vulu, ambapo Jeremiah alisema kazi inaendelea vizuri.
Dkt. Kawambwa aliyefika kwa lengo la kujionea kazi inavyokwenda ili aweze kumpatia mrejesho Waziri Mwenye dhamana Dkt. Medard Kelemani, aliyefika kitongojini hapo Febr 2 huku
akiacha agizo kwa Mkandarasi kuhakikisha anaikamilisha kazi hiyo kama ilivyopangwa.
Jeremiah alisema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha kazi inakamilika kama walivyomhaidi Waziri, na kwamba ndani ya eneo la Chasimba wana nguzo mia mbili, na nyingine miamoja watazipokea ndani ya simu nne kutoka Feb 13.
"Kazi inakwenda kwa kasi, hapa Chasimba tumeshasimamisha nguzo zaidi ya 800, matarajio yetu ni kuukamilisha mradi huu kama agizo la Waziri Kalemani alivyotutaka, kazi inakwenda vizuri tunaahidi kuikamilisha kulingana na tarehe iliyopangwa," alisema Jeremiah.
Akizungumza mbele ya msafara huo, Dkt. Kawambwa alisema kuwa Kampuni hiyo ilikabidhiwa kazi hiyo miezi kadhaa iliyopita, lakini cha kushangaza ilichelewa kufika eneo la kazi, hatua iliyomlazimu kuwasiliana na Waziri Kalemani kuhusiana na kusuasua huko.
"Baada ya kuona mradi unasuasua, nikiwa bungeni nikamweleza Dkt. Kalemani aliyekabidhiwa Wizara hiyo na Rais wetu mpendwa Dkt. John Magufuli, akaniahidi tukitoka bungeni atafika, Waziri ni muungwana sana, Feb 2 tulifika wote, leo nimekuja kuhakiki ili nimpatie mrejesho wa kazi" alisema Dkt. Kawambwa.
Nae Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake ya Wilaya ya Bagamoyo Lukhia Masenga, alimtaka Meneja huyo amjuze ni lini watafika ndani ya Kata ya Ubena, ambako kuna maeneo yalitoainishwa kufikishiwa umeme, huku akieleza kuwa pamoja na ahadi hiyo lakini hakuna nguzo hata moja.
Akijibia hilo na swali la Diwani wa Kata ya Magomeni Mwanaharusi Jarufu, Jeremiah alisema kuwa Sanzale Kata ya Magomeni litafikiwa baada ya Kitongoji cha kwa Mbwela Kata ya Kiwangwa, huku Ubena nao ikifikiwa baada ya kumalizika maeneo hayo.



No comments:
Post a Comment