Moto wa ndugu kwa mara ya kwanza utaonekana ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2019-20 ambapo Simba na Yanga zitamenyana kwa mara ya kwanza msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara.
Ukiachana na tambo ambazo zinatawala kwa kila mmoja kama ilivyo ada kwamba siku zote mwamba ngoma huvutia kwake ndivyo ilivyo kwa hawa watani wa jadi ila ndani ya uwanja itakuwa ni vita kubwa ya ndugu wa kutoka taifa moja wakionyeshana umwamba wao.
Macho na masikio ya mashabiki ni kuona ni nani atakayemfunika mwenzake huku makocha wao wakimalizia mbinu zao kuona kwamba wanabeba pointi tatu bila kujali ugumu wa mchezo huo.
Pale ambapo mataifa kutoka nje ya nchi wanapokutana mahali pengine hawa huitwa ndugu kutokana na kuunganishwa na taifa lao, sasa hapa waliopo Bongo watauweka undungu pembeni kwa muda.
Kwenye timu hizi za Simba na Yanga kuna wachezaji ambao wanatoka taifa moja na watakuwa kazini Januari 4, kila mmoja akiwa upande wake akitetea ugali wake na nafasi yake upya kwenye timu yake ya taifa ni ndugu nje ya uwanja ila watakutana kwa mara ya kwanza kutafuta pointi tatu uwanja wa taifa
No comments:
Post a Comment