Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya kigeni ya Saudia Arabia imesema hatua ya Uturuki ya kuongeza mvutano inatishia usalama na uthabiti wa Libya na ni kitisho kwa ulinzi wa kanda hiyo kwa jumla.
Hayo yanajiri wakati watu 28 wameuwawa jana katika shambulzii lililotokea kwenye chuo cha kijeshi kwenye mjini mkuu wa Libya, Tripoli.
Waziri wa Afya wa serikali yenye makao yake mjini Tripoli amesema idadi ya wahanga inaendelea kuongezeka huku ikielezwa kuwa shambulizi hilo limefanywa na vikosi vya serikali hasimu ya upande wa mashariki.
Mji wa Tripoli ulio chini ya serikali inayotambuliwa kimataifa, unakabiliwa na mashambulizi tangu mwezi Aprili kutoka vikosi vya mbabe wa kivita, Jenerali Khalifa Haftar wa jeshi la upande wa mashariki.
No comments:
Post a Comment