Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mtatiro amendika kuwa, "tofauti na maeneo mengi ya Nchi yetu, Tunduru kuna herehe 2 za kuwaaga darasa la saba, ya kwanza ni mahafali yanayoandaliwa na shule yakiwashirikisha wahitimu, wazazi wao na wanafunzi, haya ni Mahafali sahihi na hufanyika kabla ya mitihani ya darasa la 7".
Aidha Mtatiro ameongeza kuwa "Mwaka huu 2020, kila Shule ya Msingi itafanya mahafali moja tu ambayo ni rasmi na itawahusisha wazazi, Walimu, Wahitimu, wanafunzi, ndugu, jamaa na marafiki, ile mahafali ya pili ambayo hufanywa na wazazi peke yao kwa kuwafuata watoto wao shuleni wakiwa kwenye vyumba vya mtihani wa mwisho, na kutumia gharama nyingi kufurahia kutua mzigo, tumeipiga marufuku na haitafanyika tena".
No comments:
Post a Comment