Adbox

Saturday, January 4, 2020

Makada wa CCM tumbo joto,kamati za siasa zatangaziwa adhabu kali

Chama cha mapinduzi CCM kimewatahadharisha wanachama wake na makada walioanza kuzunguka katika majimbo na kata kwa nia ya kuonyesha kugombea nafasi mbali mbali za udiwani na Ubunge kabla ya wakati kutangazwa kwa mujibu wa kanuni na katiba za chama hicho.

Makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Tanzania bara Ndg,Philip Mangula amewataka wanachama na viongozi wa CCM nchini kuzingatia kanuni na taratibu za chama hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa madiwani,wabunge na Rais.

Mangula ametoa agizo hilo katika mkutano wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe uliofanyika januari 03/2020 wilayani humo kwa lengo la kutoa na kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2015 kwa mwaka wa fedha 2018-2019

Akihutubia wanachama walioshiriki mkutano huo wa kupokea taarifa amesema, kamati za siasa zitawajibika endapo ukiukwaji wa kanuni utajitokeza na kuongeza kuwa endapo wataachwa viongozi hao watahatarisha hali ya Amani na utulivu ndani ya chama.

“Naomba sana tuheshimu katiba,diwani kama kuna mtu anapita pita kwenye eneo lako na wewe ukamwachia hivyo hivyo na wewe mwenyewe ni mharifu,wilaya ijue kuwa kuna watu anapita pita huko,kwa mbunge hivyo hivyo,litakapovunjwa bunge ndio mwisho wa mbunge katika jimbo,ukijipitisha pitisha tukajua unajipitisha halafu kamati ya siasa ya wilaya inaacha unapita pita,tukigundua hilo tunaichapa kamati ya siasa,maana yake nini kila mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya anapewa onyo”alisema Philip Mangula

Awali wakisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani,mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Ally Kasinge na mbunge wa jimbo hilo Muhandisi Gelson Lwenge wamekili kupokea fedha za miradi ya maendeleo ikiwemo ya maji na elimu kutoka serikali kuu na kuzifanyia kazi kulingana na maelekezo ili kuwafikishia huduma stahiki wakazi wa wilaya hiyo ambazo awali zilikuwa kero.

Viongozi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe kupitia mwenyekiti Mzee Jassel Mwamwala, wametumia fursa hiyo kuwahimiza Wananchi kujitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la kudumu la Mpiga kura lililoanza mkoani hapo Januari mosi na kutarajiwa kuhitimishwa Januari 07/2020.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi na wanachama wa wilaya ya wanging’ombe katibu wa CCM wilayani humo Ndg, Juma Nambaila amemshukuru makamu mwenyekiti wa CCM bara kwa kuhudhuria mkutano huo na kuridhishwa na utekelezaji wa Ilani pamoja na kukumbusha ufuataji wa kanuni na sheria kwa wanachama wanaotangaza nia kuelekea uchanguzi mkuu.

Siku kadhaa zilizopita miongoni mwa habari zilizokuwa zikisambazwa mitandaoni ni pamoja na habari inayomhusu Naibu waziri wa Tamisemi Mwita Waitara aliyesikika akitangaza kuwa ni miongoni mwa watia ni 2020 endapo vikao vya CCM vya maamuzi vitaamua,huku baadhi ya wananchi wakitafsiri kwamba agizo la viongozi wakuu wa chama hicho ni kutokana na viongozi hawa kutokea hadharani.

“2020 mimi ni miongoni mwa watia nia ubunge jimbo la Tarime vijijini,na ninaomba ikitokea CCM wakinipitisha vikao vya CCM vitaamua.”alisikika Waitara katika moja ya Video mitandaoni.

Aidha mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Samwel kiboye baada ya taarifa hizo pia aliweza kujitokeza na kukemea tabia hiyo.

“Muda wa kujinadi bado Tarime sasa hivi inatuumiza sana,inamaana sasa anakwenda kuleta Makundi na mpaka sasa hivi ameshaleta makundi lakini kibaya zaidi anatumia baadhi ya vijana wanawakashfu watu,kama mwenyekiti wa mkoa wa Mara sitakubali,nasema ni marufuku hao wanaokuja wanajiita wametumwa hakuna hiyo”Alisema Kiboye

No comments:

Post a Comment

Adbox