Adbox

Sunday, January 5, 2020

Burkina Fasso: Watu 14 wamekufa kwenye mlipuko

Takriban watu 14 wengi wakiwa wanafunzi wamekufa baada ya basi walililokuwa wakisafiria kukanyaga bomu kaskazini magharibi ya Burkina Fasso wakiwa njiani kurejea shuleni baada ya mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Kulingana na msemaji wa mkoa wa Boucle du Mouhoun kulikotokea kisa hicho amesema watu wengine wanne wamejeruhiwa kutokana mlipuko huko.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo lakini makundi ya itikadi kali yenye mafungano na Al -Qaeda pamoja na kundi linalojiita Dola la Kiislamu yamekuwa yakilaumiwa kwa matukio kama hayo nchini Burkina Fas.

Vifo hivyo vimetokea ikiwa ni wiki moja baada ya watu 35 wengi wakiwa wanawake kuuwawa kwenye shambulizi lililotokea kwenye mji wa kaskazini wa Arbinda huku wanajeshi saba waliuwawa kwenye shambulizi tofauti katika kambi ya jeshi karibu na eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Adbox