Adbox

Tuesday, December 31, 2019

Wanafunzi 17,820 kupangishwa nyumba za NSSF Mtoni Kijichi Dar

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limesaini makubaliano ya awali na vyuo vya elimu ya juu vilivyopo Dar es Salaam, kwa ajili ya kuwapangisha wanafunzi nyumba zilizopo Mtoni Kijichi.

Akizungumza mara baada ya kuweka saini makubaliano hayo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio, alisema zaidi ya wanafunzi 17,820, watanufaika na nyumba hizo katika awamu ya kwanza kutoka Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam (DIT), Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Aidha aliwataka Watanzania kuchangamkia fursa ya kukopa nyumba zilizopo Toangoma na Dungu, ambazo zinafaa kwa makazi, kwa kupangishwa ama kwa kuuza.

Vile Vile, alisema uwepo wa nyumba hizi ni fursa kwa taasisi za fedha kuanza utaratibu kwa wanaotaka kupanga au kununua nyumba hizo waanze utaratibu wa kuwakopesha na ikiwezekana kwa riba maalumu ambayo itakuwa nafuu.

Alisema ni ruksa kwa Watanzania wote kununua nyumba hizo kwani ni nyingi na za aina tofauti zipo za vyumba vitatu mpaka vitano.

No comments:

Post a Comment

Adbox