Waombolezaji hao walizingira ubalozi huo uliopo kwenye eneo lenye ulinzi mkali wakiwa wamebeba bendera za kundi la wanamgambo lenye ushawishi mkubwa.
Wakati huo huo, Saudi Arabia imewalaani wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran kwa kuyashambulia majeshi ya Marekani yaliyoko nchini Iraq ambapo mkandarasi mmoja wa Marekani aliuliwa.
Wanamgambo hao walifanya mashambulio hayo wiki iliyopita. Marekani ilijibu kwa kuwashambulia kwa ndege wanamgambo hao wa Kataib Hezbollah Jumapili iliyopita.
Wanamgambo hao wa Hezbollah walikishambulia kituo cha kijeshi cha Marekani nchini Irak Ijumaa iliyopita.
Hata hivyo Waziri Mkuu wa Iraq, Adel Abdul Mahdi ameilaani pia Marekani kwa kufanya mashambilio ya ndege yaliyolenga vituo vya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran.
Amesema hatua ya Marekani inaweza kuitumbukiza zaidi Iraq katika vita vya kiwakala baina ya Marekani na Iran.
No comments:
Post a Comment