Adbox

Tuesday, December 10, 2019

Tanzania yazitaka Nchi za ACP kujitafakari upya

Tanzania imezitaka Nchi za Afrika,Caribbean na Pacific kutafakari upya kuungana na kuongeza wigo wa biashara baina ya mataifa hayo ili kujiletea maendeleo na kuheshimika mbele ya mataifa ya Ulaya na kwingineko duniani.

Hayo yamesemwa na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Prof. Palamagamba John Kabudi alipokuwa akiwasilisha ujumbe wa Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kilele cha mkutano wa tisa wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific unaofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya.

Prof. Kabudi amesema ameongeza kuwa wakati umefika sasa kwa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific kutafakari na kuacha kuzungumzia uhusiano wao wa kibiashara baina ya ACP na Ulaya na badala yake ziangalie upya namna ya kufanya biashara zenyewe kwa zenyewe na kuhakikisha kuwa umoja huo unazisaidia nchi hizo kupiga hatua mbele za kiuchumi.

Ameongeza kuwa kwa miaka 44 tangu kuanzishwa kwa ACP nchi hizo zimetumia muda mrefu kujadiliana nan chi za ulaya kuhusu mahusiano ya kibiashara na kupendekeza kuwa wakati ni sasa kwa nchi za ACP kuungana na kujenga viwanda vya kimkakati baina ya mataifa kutokana na rasilimali zilizopo ili kufanya biashara linganifu na kujijengea heshima miongoni mwa mataifa mengine yakiwemo ya bara ulaya na Amerika.

Katika Mkutano huo uliofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewasilisha ujumbe wa kuitaka jumuiya ya kimataifa nan chi za Ulaya na Marekani kuiondolea vikwazo Zimbabwe bila ya masharti yeyote ili kuliwezesha Taifa hilo kujijenga upya kutokana na sababu zilizosababisha kuwekwa kwa vikwazo hivyo kutokuwepo tena.

Ameongeza kuwa vikwazo hivyo vya kiuchumi kwa Zimbabwe vinasababisha madhara makubwa kwa uchumi wa Taifa hilo na kuwaathiri watu wasio na hatia hususani akina mama na watoto na kuitaka ACP kuungana na SADC nan chi nyingine zenye mapenzi mema kutaka kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment

Adbox