Adbox

Thursday, December 5, 2019

Sekondari ya Wasichana Loleza yang'ara kwa Milioni 900

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Loleza ya Jijini Mbeya kuzingatia masomo kwani mazingira sasa yanaruhusu kusoma bila wasiwasi kutokana na changamoto za miundombinu kutokuwepo baada ya shule kufanyiwa ukarabati Mkubwa kwa zaidi ya Milioni 900.

Ndalichako ameyasema hayo alipotembelea shule hiyo kuona ukarabati uliofanyika akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Albert Chalamila na viongozi wengine wa Mkoa na Wilaya, huku Mkuu wa Mkoa akipongeza na kuishukuru Wizara ya Elimu kwa kuwezesha ukarabati huo na kumuhakikishia waziri kuwa Mkoa umejipanga kufuatilia utunzaji wa miundo mbinu hiyo huku kuwaasa wanafunzi kuilinda.

Wakiwa katika shule hiyo pia walitembelea bwalo jipya linalojengwa na shule kwa kutumia mapato yao ya ndani. Ndalichako amempongeza Mkuu wa Shule hiyo na uongozi wote na kuwataka wanafunzi kushiriki katika kazi za mikono na miradi ya kujitegemea.

No comments:

Post a Comment

Adbox