Na Tiganya Vicent
Madiwani na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge wametakiwa kuachana na mpango waliokusudia wa kutenga Kituo cha ukusanyaji wa asali bali wafikirie wazo la ujenzi wa Kiwanda cha kusindika asali ili kuongeza thamani ya asali hiyo
Ushauri huo umetolewa juzi wilayani Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
Alisema utaratibu wa ujenzi wa Kiwanda utawasaidia wafugaji wa nyuki kupata faida kubwa na kuwa na bidhaa ambazo zinajulukiana asili yake zinazalishwa na Kiwanda cha Sikonge(Made in Sikonge)
Mwanri alisema kitendo cha kuruhusu Sikonge kugeuka kuwa sehemu ya kukusanya asali ambayo haijasindikwa utasababisha watu kutoka nje kuingia katika eneo la kukusanya asali yote na kuwaacha wafugaji wakiwa na faida kidogo huko ikienda kunufaisha maeneo mengine.
“Naona Sikonge hatuelewani mimi nazungumzia uanzishaji wa Kiwanda cha kusindika asali na kuiweka kwenye vifungashio kama vile Chupa ambazo zina nembo ya Sikonge, nyie mnafikiria kuwa na ‘collection centre’ ambapo asali itauzwa kabla ya kuongezewa thamani na kwenda kunufaisha watu wa sehemu nyingine na kuwacha watu wakiwa maskini “ alisema.
Alisema uanzishwaji wa Kiwanda utasaidia kuwapa wafugaji na wakazi wa eneo hilo kupata mtaji na teknolojia ya kisasa ya usindikaji asali na ajira na kuboresha maisha ya familia katika eneo la Sikonge na Halmashauri itapata mapato.
Thursday, December 5, 2019
RC Mwanri awataka Sikonge kujenga kiwanda cha kusindika asali
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment