Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa Zanzibar ina mengi ya kujifunza kutoka Vietnam kutokana na mafanikio makubwa yaliopatikana nchini humo chini ya Chama cha Kikomunisti cha (CPV).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo Ikulu Mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na Mjumbe na Katibu wa Kamati Kuu ya Uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) Bwana Pham Minh Chinh akiwa amefuatana na ujumbe wa viongozi kutoka Chama hicho.
Katika maelezo yake Rais Dk. Shein alisema kwamba nchi hiyo imepata mafanikio makubwa katika nyanja zote zikiwemo za kiuchumi, kijamii na kisiasa na kueleza kuwa Zanzibar itaendelea kujifunza kutoka nchi hiyo.
Rais Dk. Shein aliipongeza Vietnam kwa kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo ambao umeweza kuleta mafanikio makubwa sambamba na mahusiano kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV).
Aidha, Rais Dk. Shein alieleza kuwa ziara ya kiongozi huyo hapa nchini inaimarisha na kukuza uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Vietnam na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo Zanzibar pamoja na vyama vikuu vinavyotawala katika nchi mbili hizo.
Thursday, December 5, 2019
Rais Dk Shein asema Zanzibar ina mengi ya kujifunza kutoka Vietnam
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment