Na. Ferdinand Shayo, Arusha
Meneja wa Mkoa wa Arusha wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) ,Isaya Shekifu amewataka wanamichezo kujiunga na bima ya afya kupitia vifurushi vya bima ya afya.
Akizungumza katika ufunguzi wa bonanza la michezo liliofanyika katika viwanja vya general tyre ,amesema kuwa kwa sasa mfuko wa bima ya afya umeboresha huduma zake kupitia vifurushi vya najali afya,wekeza afya na timiza afya .
Amewataka wananchi wa Arusha kuchamkia fursa ya vifurushi kwani ni vya gharama nafuu na vimekidhi matakwa ya wananchi ya kuwa na Bima nafuu ya mtu mmoja mmoja kujipimia kwa kadiri ya mahitaji yake.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro amesema kuwa uwepo wa watu wa bima hiyo unapaswa kutumika vizuri kwa wananchi waliojitokeza kwenye bonanza hilo kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya taifa.
Gabriel amewataka wanamichezo na wakazi wa wilaya ya Arusha kuhakikisha kuwa wanakua na bima ambayo inawapa uhakika wa kupata matibabu hasa wanapougua wao ama familia zao.Isaya amesema kuwa licha ya michezo kutumika kama njia ya kujenga umoja,ushirikiano na pia kuwa ni afya hivyo wananchi wanapaswa kujiunga na bima ili waweze kutibiwa wao na familia zao .
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro amesema kuwa uwepo wa watu wa bima hiyo unapaswa kutumika vizuri kwa wananchi waliojitokeza kwenye bonanza hilo kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya taifa.
Gabriel amewataka wanamichezo na wakazi wa wilaya ya Arusha kuhakikisha kuwa wanakua na bima ambayo inawapa uhakika wa kupata matibabu hasa wanapougua wao ama familia zao.
Alisema kuwa wilaya ya Arusha imekua na hamasa kubwa katika kujiunga na bima ya Afya na wanaendelea kuhamasisha wananchi kuona umuhimu wa kujiunga na NHIF kwa faida ya afya zao.
Monday, December 9, 2019
NHIF yawahakikishia wanamichezo huduma za Bima ya Afya
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment