Adbox

Monday, December 9, 2019

Alichosema Naibu Spika kwenye Mkutano Mkuu wa Simba SC

Naibu Spika wa Bunge ndiye aliyekuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano Mkuu wa Klabu ya Simba ulofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Nyerere.

Katika mkutano huo amesema uongozi kama Simba uliyoko madarakani kwa sasa ndio wanautaka Wanasimba na kuzitaka timu nyingine kuiga.

“Nimeona jana mambo mazito kabisa. Nimefurahi kusikia katika moja ya mipango kuanzisha Simba Academy, hili sio muhimh kwa Simba bali hata kwa nchi. Nawapongeza sana viongozi kuona umuhimu wa kusaidia vijana wadogo”.

“Sisi kama mashabiki lazima tusiwe wa kwanza kuwakatisha tamaa viongozi wetu, tusiwe wa kwanza kuwasema vibaya, tuwaunge mkono katika kuipeleka timu yetu next level”.

“Mimi ni sehemu ya wabunge, na wabunge wengi ni Simba, yupo kule Mhe. Spika, yupo pia Mhe. Waziri Mkuu niwambie tu kule wengi ni Simba” amesema Dkt. Tulia.

No comments:

Post a Comment

Adbox