Mashabiki wa Simba SC leo wamejitokeza kwa wingi kushuhudia uwanja wa timu hiyo wa nyasi bandia ukiwa umekamilika maneneo ya Bunju, Dar es Salaam.
"Kwanza namshukuru Mwenyekiti wa Bodi kwa kututengezea uwanja. Inahitaji moyo sana kufanya kazi ya kujitolea hata sisi miaka ya nyuma tulijenga majengo kwa kujitolea kwa kubeba matofali kichwani na yeye sasa anaendeleza hilo. Na sisi tunampongeza tupo nyuma yake kumuunga mkono”- Mwenyekiti Mstaafu Hassan Dalali.
“Kazi mnayofanya viongozi sasa mnaiona, tusaidiane kuifikisha timu tunapotaka. Nawaomba tushirikiane na wenzetu. Nina imani mwaka huu ubingwa tunachukua.”- Mchezaji na kocha wa zamani, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’.
“Tunashukuru kwa viwanja hivi, vitatuongezea nguvu kuhakikisha tunashinda. Nawashukuru viongozi pamoja na mwekezaji, najua wamepitia vikwazo vingi lakini wameweza kufikia hii hatua. Nawashukuru mashabiki wetu kwa kujitokeza kwenye eneo hili na viwanjani au tukisafiri mikoani. Nawashukuru sana, nawaomba muendelee kuwa na upendo kwa wachezaji na viongozi.”- Nahodha John Bocco.
Saturday, December 7, 2019
Mashabiki wa Simba SC wajitokeza kwa wingi uwanja wa Bunju
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment