Na Ferdinand Shayo-Arusha
Tanzania imekua moja kati ya nchi chache barani Afrika zilizofanikiwa kupunguza maambukizi ya kifua kikuu sugu kutokana na juhudi zilizofanyika za kuanzishwa vituo vingi vya huduma za upimaji na matibabu ya kifua kikuu katika ngazi ya kitaifa, mkoa, wilaya na kata.
Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Kambi amesema hayo wakati akifungua mkutano wa wataalamu wa afya unaolenga kutathimini mpango wa kutomeza kifua kikuu na ukoma wa miaka mitano unaomalizika 2020 ambapo Tanzania imeweza kubaini wagonjwa wapya asilimia 53 na kuwapatia matibabu juhudi ambazo zinapaswa kuongeza kasi ili kutokomeza magonjwa hayo.
Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo jamii, jinsia,Wazee na watoto, Dr.Leonard Subi amesema kuwa serikali imetoa hadubini 800 za kupima kifua kikuu katika vituo vya afya ili kusogeza karibu huduma za upimaji kwa wananchi hususani walioko vijijini.
Meneja wa Mradi wa kutokomeza kifua kikuu na ukoma Dr.Beatrice Mtayoba amesema kuwa ziko halmashauri 16 ambazo ziko nyuma katika kupiga vita ugonjwa wa ukoma hivyo serilkali imeweka msukumo mkubwa na kutoa elimu ili kukabiliana na ugonjwa wa ukoma.
Mratibu wa Masuala ya Kifua kikuu katika Maeneo ya Migodi, Dr.Allan Tarimo amesema kuwa maeneo ya migodini yanakabiliwa na changamoto ya idadi kubwa ya wagonjwa wa kifua kikuu hivyo serikali imeamua kusogeza huduma za upimaji katika maeneo ya machimbo ikiwemo Mererani ambako kuna wagonjwa wengi ukilinganisha na maeneo ya makazi ya watu ya kawaida.
Kwa upande wake Shuhuda Anorld Ntahondi ambaye aliwahi kupata ugonjwa wa kifua kikuu ameeleza jinsi ambavyo alivyokubwa na adha hiyo na awali alifika kwa waganga wa kienyeji baada ya hali kuwa mbaya alifika hospitali na kupatiwa matibabu na kwa sasa amepona.
Monday, November 25, 2019
Tanzania yapunguza Maambukizi ya Kifua Kikuu Sugu
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment