Adbox

Monday, November 25, 2019

Jopo la Majaji watatu kutumia siku 16 kusikiliza mashauri 29 Zanzibar

Mwenyekiti wa Jopo la Majaji wa Mahama ya rufaa ambayo itaanza kikao chake leo hii mjini Unguja Jaji Agostona Mahija akikagua gwaride  kabla ya kuanza kwa kikao hicho mjini Unguja leo.

Jumla ya mashauri 29 yanatarajiwa kuwasilishwa na kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa ambayo inaanza leo Jumatatu Novemba 25 hadi Desemba 11, 2019 Kisiwani Unguja, Zanzibar. 

Hayo yamesemwa leo  na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa Amir Khamis Msumi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kikao hicho cha wiki tatu kimepanga kusikiliza mashauri yote na ikiwezekana kuyatolea uamuzi.

Amesema katika mashauri yote 29 yaliowasilishwa kwenye Mahakama hiyo yamegawika katika makundi matatu tofauti.

Akifafanua makundi hayo amesema mashauri ya rufaa  ni 12, mashauri ya jinai matatu, mashauri ya madai 11 na maombi ya jinai ni matatu.

Msumi amesema kikao hicho cha wiki tatu kitaongozwa na majaji watatu ambapo Mwenyekiti wao atakuwa Jaji Agostona Mahija akisaidiana na Jaji Gerad  Ndika pamoja na Jaji Rehema Kerefu.

No comments:

Post a Comment

Adbox