Na. Ahmad Mmow, Newala
Chama kikuu cha ushirika cha Tandahimba and Newala Co-operative Union( TANECU) mkoani Mtwara, jana kiliuza korosho za wakulima zenye uzito wa tani 13,181 katika mnada wa kwanza kwa msimu wa 2019\2020 uliofanyika mjini Newala.
Katika mnada huo ambao ulihudhuriwa na kushuhudiwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa bei ya juu ilikuwa shilingi 2,526 kwa kilo moja huku bei ya chini ikiwa shilingi 2,468.
Taarifa ya makusanyo ya Korosho na kiasi kilichoingizwa katika mnada iliyosomwa na meneja mkuu wa TANECU Ltd ,Mohammed Nassoro ilibainisha kuwa Korosho zilizouzwa zilikuwa kwenye maghala makuu ya TANECU yaliyopo Newala na Tandahimba na Agrofocus Newala.
Ilieleza kwamba katika ghala la Agrofocus ziliuzwa tani 194, ghala la TANECU Newala ziliuzwa tani 6,303 na ghala la TANECU Tandahimba ziliuzwa tani 6,682.
Baada ya kaimu mkurugenzi wa bodi ya korosho Tanzania, Frances Alfred kutoa taarifa ya bei ya korosho katika soko la Dunia hadi kufikia jana kuwa Korosho zinauzwa kwa kati ya shilingi 2,440 hadi shilingi 2,740. Wakulima walikubali ziuzwe kwa bei zilizofikiwa na wanunuzi.
Aidha mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa aliwasisitiza viongozi wa chama kikuu hicho na bodi ya korosho Tanzania kuharakisha mchakato wa malipo ili wakulima walipwe fedha zao kwa muda muafaka.
Katika mnada huo kampuni 28 zilijitokeza kuomba kununua, ambapo hitaji la kampuni hizo lilikuwa ni tani 40,000. Hatahivyo korosho zilizokusanywa hadi tarehe 29, mwezi huu( Oktoba),mwaka 2019 na kuuzwa kwenye mnada huo ni hizo tani 13,181.
Friday, November 1, 2019
TANECU yauza tani 13,181 za Korosho
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment