Adbox

Wednesday, November 27, 2019

Taarifa za upimaji wa Ardhi kuhifadhiwa kitaalam zaidi

Mabadiliko ya sayansi na teknolojia hapa nchini Tanzania na duniania kote yamebadilisha na kuboresha utendaji kazi kwenye Mashirika, Taasis na ofisi za umma pamoja na za watu binafsi. Mafanikio makubwa yanayoletwa na matumizi ya teknolojia ni pamoja na kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii na kupunguza gharama za huduma hizo.

Haya yalisemwa na balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania Bwana Tae – ick Cho alipokuwa akitoa salamu za ufunguzi na shukrani kwenye mkutano uliofanyika jana jijini Dar es Salam kuhusu teknolojia ya ukusanyaji taarifa za kijeografia kwa ajili ya kurahisisha upimaji ardhi nchini kwa kitaalam Geospatial Information Road Show zitakazotumika kurahisha upimaji wa ardhi pamoja na huduma nyingine za jamii.

Mkutano huo ulihusisha wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Makampuni yanayohusika na upimaji kutoka nchini Korea, ikiwa lengo ni kubadilishana uzoefu kuhusu namna bora ya kuhifadhi na kutunza taarifa za masuala ya upimaji na kupunguza gharama ya kutekeleza kazi hiyo.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo wa siku tatu, Balozi Tae – ick Cho aliwashukuru wataalamu Kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ushirikiano wao pamoja na wadau wote ambao wamekuwa wakishirikiana pamoja kuona ni jinsi gani wanaweza kutumia teknolojia ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa za Kijeografia ambazo mwisho wa siku zitatumika kwenye huduma mbalimbali za kijamii lakini kubwa zaidi ikiwa ni masuala ya upimaji na utunzaji wa taarifa hizo kwa usalama.

Nae Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Bwana Hamdouny Masour akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi alisema, Tanzania itafaidika na mambo mengi sana kupitia teknolojia mpya ya Geospatial Information Road Show na hasa kuongeza miundombinu ya masuala ya upimaji ardhi hapa chini.

No comments:

Post a Comment

Adbox