Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, anatarajiwa kuchukuwa uongozi wa shirika la umoja wa nchi za Afrika (AU) kama mwenyekiti ifikapo January 2020.
Hii ni baada ya kamishna wa shirika hilo lenye wanachama 55 barani Afrika, Moussa Faki Mahamat na mafisa wengine wa ngazi za juu katika AU, kukamilisha ziara ya siku mbili nchini Afrika Kusini huku wakifanya mazungumzo na Rais Ramaphosa pamoja na maafisa wa serikali nchini humo.
Taarifa kutoka shirika la AU lilisema kuwa viongozi hao wawili walijadili mikakati na maswala ambayo Afrika Kusini itazingatia itakapochukua usukani kama mwenyekiti wa AU, huku Ramaphosa akisisitiza umuhimu wa kupatikana kwa suluhu na amani katika nchi ya Libya.
Monday, November 25, 2019
Rais wa Afrika Kusini kushika uongozi AU
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment