Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuharakisha ujenzi wa hospitali ya Wilaya Chamwino mkoani Dodoma na kukosoa ushauri uliotolewa na Wakala wa Majengo nchini (TBA).
Ametoa kauli hiyo leo baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo utakaogharimu Sh3.4 bilioni huku akimtaka Mkuu wa JKT, Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwaweka mahabusu wataalamu wa TBA watakaochelewesha ujenzi huo.
“Hizi hela zimetoka siku nyingi maendeleo ya kazi hayaridhishi nasema kweli au uongo?” amehoji Magufuli huku akisema awali zilitolewa Dola 1000 za Marekani sawa na Sh2.4 bilioni huku Hazina kukiwa na salio la Sh995 milioni.
Kiongozi mkuu huyo wa nchi amesema awali ujenzi huo ulitolewa kwa TBA lakini walikuja na makisio ya Sh6 bilioni kiasi alichosema ni kikubwa kuliko makisio ya Serikali.
“Sasa hospitali za wilaya tunaweka Sh1.5 bilioni, hapa maana yake ni kama hospitali mbili na nusu. Vituo vya afya tunatumia Sh500 milioni na panakuwa na majengo matano hadi sita. Kwa nini hapa eneo moja iwe Sh6 bilioni.”
“Sasa kwa sababu mmenikaribisha kuweka jiwe la msingi na mimi mwenyewe niko hapa hata nikiwa nafanya mazoezi tutajuana vizuri. Kwa nini mlichelewesha ujenzi,” amesema Magufuli.
Friday, November 22, 2019
Rais Magufuli atoa agizo kuhusu ujenzi wa Hospitali Chamwino
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment