Rais John Magufuli amemtaka Mkurugenzi wa Igunga kuhakikisha kesho anaitisha kikao cha dharura cha madiwani Igunga kwa ajili ya kubatilisha matumizi ya fedha kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja ambazo zilipitishwa na baraza la madiwani kujenga mitaro.
Rais Magufuli amesema amewashangazwa na uamuzi wa madiwani hao kwa kutozipa kipaumbele barabara za mitaa zinazolalamikiwa na wananchi wengi na badala yake wameona mitaro ndiyo kipaumbele chao.
"Sasa madiwani mnaomba fedha kwaajili ya matumizi ya mitaro kweli, kwanini msingepitisha kwaajili ya ujenzi wa barabara, yaani fedha ziletwe kutoka serikali kuu. Mmkurugenzi naomba utekeleze maagizo niliyokupa la sivyo nitaagiza hizo fedha zisiletwe," Rais Magufuli.
Wednesday, November 27, 2019
Rais Magufuli akerwa na Bilioni 1 kutengeneza Mitaro Igunga
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment